Header Ads

Diego Simeone: Tumepambana Na Tumefanikiwa

Bosi wa kikosi cha Atletico Madrid Diego Simeone wametoa pongezi kwa wachezaji wake, kufuatia ushindi wa mabao manne kwa mawili waliouvuna mbele ya wenyeji wao Bayer Leverkusen usiku wa kuamkia hii leo huko nchini Ujerumani.
Simeone aliwaambia waandishi wa habari kuwa, wachezaji wake walionyesha ujasiri wa kupambana na kupata matokeo mazuri ugenini, jambo ambalo anaamini litakisaidia kikosi chake kwenye mchezo wa mkondo wa pili utakaochezwa majuma mawili yajayo mjini Madrid.
Meneja huyo kutoka Argentina, alisema ni vigumu kupata matokea mazuri ugenini, lakini upambanaji wa kikosi chake uliwezesha jambo hilo kuwa rahisi.

Mabao ya Atletico Madrid katika mchezo huo uliounguruma BayArena yalifungwa na Saul Niguez, Antoine Griezmann, Kevin Gameiro na Fernando Torres huku mabao ya kufutia machozi ya wenyeji yakipachikwa na Karim Bellarabi na Stefan Savic aliyejifunga mwenyewe.

No comments

Powered by Blogger.