Header Ads

Di Maria Aombwa Kurudi Hispania

Mshambuliaji wa mabingwa wa soka nchini Hispania FC Barcelona Lionel Messi amemtaka Angel Di Maria kufikiria kurejea nchini humo na kujiunga nae Camp Nou.

Messi amemuomba Di Maria kufanya hivyo, kutokana na kiwango chake kubadilika kwa kiasi kikubwa, tangu alipoondoka Real Madrid na kutimkia Man Utd na kisha PSG.

Kwa mujibu wa baadhi ya vyombo vya habari vya Hispania, Messi amekua akifanya ushawishi wa kumtaka Di Maria kurejea Hispania, tangu FC Barcelona walipokutana na dhoruba ya kufungwa mabao manne kwa sifuri kwenye mchezo wa 16 bora wa ligi ya mabingwa barani Ulaya juma lililopita.

Di Maria alifunga mabao mawili miongoni mwa mabao manne yaliyoiweka pabaya FC Barcelona katika harakati za kutinga hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu huu.

Di Maria tayari ameshaifungia mabao manane PSG katika michezo 29 aliyocheza msimu huu.

No comments

Powered by Blogger.