Header Ads

David Mbevi: Hakuna Askari Wa Kenya Aliyeuawa Na Wapiganaji Wa Al Shabaab


Serikali ya Kenya imesema hakuna askari wake aliyeuawa baada ya wapiganaji wa kundi la Al Shabaab la Somalia kuvamia kambi ya polisi iliyoko kaskazini mwa nchi hiyo.

Ofisa wa serikali ya kanda David Mbevi amesema, watu waliokuwa na silaha wamechukua mashine nne za kusajili wapiga kura mali ya Tume ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC), bunduki mbili za polisi, na bunduki moja ya askari wa wanyamapori iliyokuwa imehifadhiwa kwenye chumba cha silaha.


Wapiganaji wa kundi la Al Shabaab ambao wamekiri kuhusika na shambulizi hilo pia walivunja mnara wa kampuni ya huduma za simu ya Safaricom.

No comments

Powered by Blogger.