Header Ads

China Yapongeza Mazungumzo Ya Amani Msumbiji

Tokeo la picha la mozambique Flag

Balozi wa China nchini Msumbiji Su Jian amepongeza mazungumzo kati ya rais Filipe Nyusi wa Msumbiji na kiongozi wa chama cha upinzani Renamo Bw. Afonso Dhlakama.

Su amesema serikali ya China inafurahia kufanyika kwa mazungumzo hayo yatakayoiletea Msumbiji makubaliano ya amani ya kudumu. Ameongeza kuwa China iko tayari kuiunga mkono Msumbiji katika juhudi za kurejesha amani na utulivu kwa wananchi wake.

Katika sherehe ya siku ya mashujaa ya Msumbiji iliyofanyika wiki iliyopita, rais Nyusi alisema awamu ya kwanza ya mazungumzo imemalizika, na awamu ijayo inatarajiwa kufanyika wiki hii.

Bw. Dhlakama amesema katika mazungumzo hayo, watajadili masuala ya jeshi na ugatuzi.

No comments

Powered by Blogger.