Header Ads

China Na Msumbiji Zaahidi Kupanua Ushirikiano


China na Msumbiji zimeahidi kupanua ushirikiano wa kunufaishana katika maeneo mbalimbali. 

Ahadi hiyo imetolewa wakati mwenyekiti wa Baraza la mashauriano ya kisiasa la China Bw. Yu Zhengsheng alipokutana na spika wa bunge la Msumbiji Bibi Veronica Macamo ambaye yuko kwenye ziara ya siku tano nchini China.

Bw. Yu amesema China inapenda kushirikiana na Msumbiji katika kuendeleza uhusiano wa pande mbili na kuhimiza utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa mwaka 2015 katika mkutano wa kilele huko Johannesburg ambapo China iliahidi kutenga dola bilioni 60 katika miaka mitatu ijayo ili kuimarisha uhusiano na Afrika.

Bibi Macamo amesema Msumbiji inaishukuru China kwa msaada wa muda mrefu tangu nchi hiyo ipate uhuru mwaka 1975, na kueleza matumaini yake kuwa uhusiano kati ya pande mbili utaimarishwa zaidi.

No comments

Powered by Blogger.