Header Ads

Cheick Tiote Akimbilia China

Tokeo la picha la Cheick Tiote

Kiungo kutoka nchini Ivory Coast Cheick Tiote amejiuinga na klabu ya ligi daraja la pili nchini China ya Beijing Enterprises Group FC akitokea Newcastle Utd ya England.

Tiote anaondoka St James' Park huku akiacha kumbukumbu kucheza michezo 139 tangu alipojiunga na Newcastle Utd Agosti 2010 akitokea FC Twente ya nchini Uholanzi.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 30, alikuwa na wakati mgumu wa kucheza katika kikosi cha kwanza kwa msimu huu, kwani mpaka anaondoka alibahatika kujumuishwa kikosini mara tatu.


Tiote alikua sehemu ya wachezaji wa timu ya taifa ya Ivory Coast waliotwaa ubingwa wa Afrika mwaka 2015, kwa kuifunga Ghana kwa changamoto ya mikwaju ya penati.

No comments

Powered by Blogger.