Header Ads

Burundi Yawataka Wakimbizi Wake Kurudi NyumbaniSerikali ya Burundi imeanzisha kampeni ya kuwataka raia wake kurudi nyumbani licha ya hali ya kisiasa nchini humo kutotulia.

Maofisa wa serikali ya Burundi wameanza juhudi za kuwashawishi warundi elfu 45 waliokimbilia Uganda kuepuka vurugu nchini mwao.

Waziri wa wa mambo ya ndani na elimu ya uraia wa Burundi Bw Pascal Brandagiye amewaambiwa waandishi wa habari nchini Uganda kuwa serikali ya Burundi inafanya juhudi kurudisha amani na kuleta malendeleo.

Waziri anayeshughulikia majanga, wakimbizi na uokoaji wa Uganda Bw Hillary Onek amesema hali ya Burundi inaboreka, na kuwataka wakimbizi warudi nyumbani kwa hiari.

Kuna jumla ya wakimbizi laki 3.27 waliokimbilia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, Rwanda, Tanzania, Uganda na Zambia. Ujumbe wa serikali ya Burundi utatembelea nchi zote kuwashawishi warudi nyumbani.

No comments

Powered by Blogger.