Header Ads

Bunge La Rwanda Lapitisha Sheria Kukifanya Kiswahili Kiwe Lugha Rasmi


Wabunge wa Rwanda jana wamepitisha sheria kukichukulia Kiswahili kuwa lugha rasmi sambamba na Kiingereza, Kifaransa na Kinyarwanda.

Hatua hiyo inamaanisha kwamba lugha ya Kiswahili itatumika kwenye shughuli za kiutawala ikiwa ni pamoja na kwenye baadhi ya nyaraka za serikali.

Waziri ya michezo na utamaduni wa Rwanda Bibi Julienne Uwacu amesisitiza umuhimu wa hatua hiyo akisema inakidhi matakwa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC ya kukifanya Kiswahili kuwa moja ya lugha rasmi. Pia itatoa fursa kwa wanyarwanda kunufaika na mafungamano ya kiuchumi.

Kufuatia kupitishwa kwa sheria hiyo, lugha hiyo itaanza kutumiwa mashuleni hatua kwa hatua.

No comments

Powered by Blogger.