Header Ads

Bunge La Ethiopia Lapitisha Makubaliano Ya Mkopo Wa Muundombinu Na Benki Ya China


Bunge la Ethiopia limepitisha makubaliano ya mkopo wa dola milioni 250 za kimarekani yaliyosainiwa na Benki ya Exim ya China kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu nchini humo.

Makubaliano hayo yaliyopitishwa na baraza la chini la bunge la nchi hiyo yatahusu ugavi na ujenzi wa miradi ya usafirishaji wa umeme katika sehemu ya kusini ya nchi hiyo.

Makubaliano yaliyosainiwa mwezi wa Disemba nchini China yana sehemu kuu mbili, sehemu ya kwanza ni mkopo wa dola milioni 195 za kimarekani zitakazotumiwa kujenga mtandao wa umeme, na sehemu ya pili ni mkopo wa dola milioni 54 za kimarekani kwa ajili ya vituo vya usambazaji umeme.

No comments

Powered by Blogger.