Header Ads

Bruno Soriano: Mwamuzi Ametunyonga

Tokeo la picha la Bruno Soriano

Kiungo wa klabu ya Villarreal Bruno Soriano amegeuka mbogo na kumtaja mwamuzi wa mchezo wao wa jana dhidi ya Real Madrid kuwa chanzo cha kupoteza point tatu kwenye uwanja wao wa nyumbani wa El-Madriga.

Bruno amefikia hatua hiyo, kwa kudai mwamuzi aliwazawadia Real Madrid penati kwa makusudi, huku akisingizia cha aliushika mpira kwa makusudi katika eneo la hatari.

"Ilionekana wazi katika picha za televisheni, sikufanya kusudio kuushika mpira, bali mpira ulikuja sehemu ya mkono wangu lakini cha kushangaza mwamuzi akawazawadia penati, hii sio haki kabisa.

"Tulicheza vizuri wakati wote, lakini kwa kitendo cha wapinzani wetu kupewa penati tukiwa mbele mabao mawili kwa moja, kilituumiza sana na kilitushusha.

"Kwetu sisi ilikua ni siku nzuri na tuliamini tunashinda mchezo huu, lakini mwamuzi aliamua anayoyajua yeye na ametugharimu kwa kiasi kikubwa.” Alisema Bruno

Katika mchezo huo Villareal walitangulia kupata mabao mawili ya kuongoza kupitia kwa Manuel Trigueros na Cedric Bakambu lakini Real Madrid walijitahidi na kupata bao la kwanza kupitia kwa Gareth Bale kabla  Cristiano Ronaldo hajawasazisha kwa njia ya penati na Alvaro Morata akaongeza bao la ushindi.

No comments

Powered by Blogger.