Header Ads

Borussia Dortmund Yashindwa Kuunguruma Ureno

Tokeo la picha la benfica 1-0 Borrusia Drtmund
Mabingwa wa soka nchini Ureno klabu ya Sport Lisboa e Benfica wamepata ushindi mwembamba wa bao moja kwa sifuri dhidi ya wawakilishi wa Ujerumani kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya Borussia Dortmund.
Sport Lisboa e Benfica walipata ushindi huo wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani wa da Luz kupitia kwa Konstantinos Mitroglou katika dakika ya 18.
Hata hivyo mshambuliaji kutoka nchini Gabon Pierre-Emerick Aubameyang alishindwa kuipatia bao la kusawazisha klabu yake ya Borussia Dortmund kwa kukosa penati katika dakika ya 58.
Kwa matokeo hayo bado inaonyesha mchezo wa mkondo wa pili wa hatua ya 16 bora, ambapo Borussia Dortmund watakua nyumbani majuma mawili yajayo, bado ni mgumu.
Michuano hiyo inaendelea tena hii leo kwa michezo miwili kuchezwa ambapo:
Bayern Munich Vs Arsenal

Real Madrid Vs SSC Napoli 

No comments

Powered by Blogger.