Header Ads

Benki Za ETI Na Afreximbank Kufadhili Miradi Binafsi Na Shughuli Za Biashara Barani Afrika

Tokeo la picha la Africa

Benki ya ETI na Benki ya Exim ya Afrika zimesaini makubaliano yanayolenga kufadhili miradi ya sekta binafsi na shughuli za biashara barani Afrika.

Benki ya ETI imetoa taarifa ikisema, makubaliano hayo yatazingatia shughuli maalum ikiwemo biashara na uwekezaji katika nchi wadau wa benki ya Exim ya Afrika, ambako benki ya ETI pia imeanzisha shughuli.

Taarifa hiyo imesisitiza kuwa ushirikiano huo wa kunufaishana kati ya benki hizo mbili utaunga mkono juhudi za kuhimiza biashara ya ndani barani Afrika, kusukuma mbele maendeleo ya viwanda na maendeleo ya uuzaji bidhaa katika nchi za nje.

Mbali na hayo, ushirikiano huo utaimarisha uongozi kwenye usimamizi wa fedha za biashara barani Afrika, lengo kuu likiwa ni kuleta mageuzi barani humo.

No comments

Powered by Blogger.