Header Ads

Benki Ya Dunia: Kutokuwa Na Uhakika Wa Sera Kunachangia Kukwamisha Ukuaji Wa Biashara

Tokeo la picha la world Bank

Utafiti wa kisera uliofanywa na Benki ya dunia unaonyesha kuwa ongezeko la biashara linakwamishwa kwa sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kutokuwa na uhakika wa sera.

Imefahamika kuwa mwaka jana ongezeko la biashara duniani lilikuwa ni asilimia moja tu, likiwa ni dhaifu ikilinganishwa na asilimia 2 na 2.7 za miaka iliyotangulia.

Utafiti huo pia umeonyesha kuwa mwaka jana ongezeko dhaifu la biashara limeonekana kwenye nchi zilizoendelea na masoko yanayoibuka, lakini mwaka juzi, biashara dhaifu ilionekana kwenye nchi zenye mapato ya juu na zinazoendelea.

Wachumi wa Benki ya dunia wamesema wenye utafiti huo kuwa kutokuwa na uhakika wa sera Ulaya na Marekani kumekuwa na athari hasi kwenye biashara, na hivyo kupunguza ongezeko la jumla la ukuaji wa uchumi wa dunia.

No comments

Powered by Blogger.