Header Ads

BASATA Wamuhoji Nikki Mbishi

Tokeo la picha la Nikki Mbishi

Msanii wa muziki wa hip hop Nikki Mbishi amedai amepokea taarifa ya kuitwa na Baraza la Sanaa Tanzania ‘BASATA’ kwajili ya mazungumzo kuhusu wimbo wake uitwao ‘I am sorry JK’.

Rapper huyo amedai aliitwa toka February 9 lakini alichelewa kupokea taarifa kwa kuwa alisafiri kwajili ya mazishi ya mama yake mkubwa.

Nikki kupitia Instagram yake aliweka wazi ujumbe uliotumwa na BASATA kumtaka afike ofisini kwao kwa kutoa maelezo zaidi juu ya wimbo huo.

Ujumbe umesema hivi  “Habari za jioni? Tafadhali fika bila kukosa BASATA kesho 10/02/2017 saa tatu kuzungumzia mustakabali wa wimbo wako wa ” I AM SORRY JK”
Nikki aliomba aripoti katika ofisi hizo tarehe 13  kutokana na kuchelewa kufikiwa na ujumbe huo.

''Unadhani nini kitatokea?Mi sifahamu ninachofahamu ni itika wito kataa neno.
Asanteni na Mungu awabariki nyote''. Nikki alimaliza kwa kusema hayo kupitia akaunti yake ya instagram.

No comments

Powered by Blogger.