Header Ads

Baraza La Kusimamia Mfumo Wa Utoaji Leseni Zanzibar (Blrc) Latoa Mafunzo Kwa Kamati Ya Baraza La Wawakilishi Ya Fedha, Biashara Na Kilimo.

 Mwenyekiti wa Baraza la Kusimamia Mfumo wa Utoaji wa Leseni Zanzibar Vuai Mussa Vuai akimkaribisha Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali kufungua mafunzo ya siku moja ya Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi yaliyofanyika Ofisi ya Baraza Malindi, Mjini Zanzibar. 

 Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali akifungua mafunzo ya siku moja ya wajumbe wa Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi yaliyoandaliwa na Baraza la Kusimamia Mfumo wa Utoaji Leseni katika Ofisi yao iliyopo Malindi Mjini Zanzibar.

 Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi wakimsikiliza Waziri wa Fedha Balozi Amina Salum alipokuwa akifungua mafunzo ya siku moja yaliyofanyika Ofisi ya Baraza hilo Malindi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi Yussuf Hassan Iddi ambae ni muwakilishi wa Jimbo la Fuoni akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi baada ya kufungua mafunzo ya siku moja ya Kamati hiyo.Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

No comments

Powered by Blogger.