Header Ads

Baraza La Chini La Bunge La Uingereza Lapitisha Rasmi Mswada Wa Brexit

Tokeo la picha la England parliament

Baraza la chini la Bunge la Uingereza limepiga kura kupitisha rasmi mswada kuhusu Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya, ambao unampa mamlaka waziri mkuu wa nchi hiyo Bibi Theresa May kuanzisha mchakato wa kujitoa Umoja wa Ulaya.

Mswada huo utawasilishwa kwenye Baraza la juu la Bunge na unatarajiwa kujadiliwa kuanzia tarehe 20, lakini ratiba ya kuupigia kura bado haijapangwa.


Kabla ya hapo serikali ya Uingereza ilisema itaanzisha rasmi mchakato wa kujitoa Umoja wa Ulaya kabla ya mwisho wa mwezi Machi.

No comments

Powered by Blogger.