Header Ads

Baraza Kuu La UN Laomboleza Kifo Cha Vitaly Churkin

Tokeo la picha la Vitaly Churkin

Baraza kuu la UN laomboleza kifo cha balozi wa Russia katika Umoja huo Vitaly Churkin.

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa jana liliomboleza kifo cha balozi wa Russia katika umoja huo Vitaly Churkin, saa chache baada ya kutangazwa kufariki dunia. 

Balozi Churkin alikuwa mjumbe wa kudumu wa Russia katika Umoja wa Mataifa tangu mwaka 2006, alifariki dunia jana kutokana na ugonjwa wa moyo mjini New York, akiwa na umri wa miaka 64.

No comments

Powered by Blogger.