Header Ads

Askari Wanane Wa Somalia Wauawa Katika Mapambano Dhidi Ya Kundi La Al-Shabaab

Tokeo la picha la police in somalia

Askari wasiopungua wanane wa jeshi la Somalia wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa kwenye mapambano na wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab katika maeneo ya Warmahan na Tihsile, kusini mwa Somalia.

Naibu mkuu wa eneo la Lower Shabelle anayeshughulikia mambo ya fedha Abdifitah Abdulle Yusuf amesema wapiganaji wa Kundi la Al-Shabaab walishambulia jeshi la serikali na kuwaua askari wanane, wakiwemo makamanda wawili waandamizi. 

Wapiganaji wawili wa Al-Shabaab waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Bw Abdulle ameongeza kuwa makamanda hao wawili waliuawa kwenye mlipuko wa bomu la kutegwa ardhini, walipokuwa njiani kuwapatia msaada wanajeshi wenzao walioshambuliwa kwenye maeneo hayo.

No comments

Powered by Blogger.