Header Ads

Asamoah Gyan Aingia Matatani Falme Za Kiarabu

Tokeo la picha la hair style of asamoha Gyan

Nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ghana Asamoah Gyan ametajwa kuwa sehemu ya wachezaji zaidi ya 40 wanaocheza ligi ya soka Falme za kiarabu, ambao wametakiwa kurekebisha aina ya kunyoa nywele zao.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31, anaitumikia klabu ya Al Ahli yenye maskani yake makuu Dubai, iliyomsajili kwa mkopo akitokea Shanghai SIPG ya china.

Sheria ya dini ya kiislamu ambayo imehusishwa kwenye kanuni za ligi ya falme za kiarabu, imekua msumeno kwa wachezaji wanakwenda kinyume na maadili.

Kanuni hiyo hutoa mwanya hadi kwa waamuzi kuwaamuru wachezaji kurekebisha baadhi ya mambo kabla ya mchezo kuanza, ili kulinda heshima na tamaduni za kiislamu katika nchi za falme za kiarabu.

Asamoah yupo kwenye hatari ya kutakiwa kunyoa nywele zake ambazo amezitengeneza kwa muonekano tofauti, ambao hauendani na kanuni zinazozuia ukikwaji wa maadili.

Mwaka 2012 mlinda mlango wa Waleed Abdullah alitakia kunyoa nywele zake kabla ya mpambano kuanza, jambo ambalo lilifanyika kwa kuzingatia kanuni za ligi ya Saudi Arabia.


Kuundwa kwa kanuni hiyo kumetokana na hofu iliyotanda katika nchi za Falme za kiarabu kwa kuwatazama watoto ambao wanahofiwa kuiga tamaduni za mataifa mengine, ambazo mara nyingi hupelekwa katika nchi hizo na wageni.

No comments

Powered by Blogger.