Header Ads

Arsene Wenger Ahofia Kuongeza Majeruhi

Tokeo la picha la Sutton Unites Vs Arsenal

Bosi wa kikosi cha Arsenal Arsene Wenger, hatowatumia wachezaji wanaunda kikosi cha kwanza katika mchezo wa mzunguuko wa 16 bora wa kombe la FA dhidi ya Sutton United utakaochezwa baadae hii leo.

Meneja huyo kutoka nchini Ufaransa, amethibitisha taarifa hizo kwa kuamini wachezaji atakaowatumia leo, watakua na nguvu za kutosha kupambana na Sutton United ambayo inashiriki madaraja ya chini nchini England.

Hata hivyo Wenger ameonyesha wasiwasi wa kuwatumia wachezaji wa kikosi cha kwanza kwenye mchezo huo kwa kusema, anahofia sehemu ya kuchezea ya uwanja wa Gander Green Lane ambayo sio nzuri na huenda ikawa kichocheo cha kuongeza majeruhi.


Miongoni mwa wachezaji wanaopewa nafasi kubwa ya kucheza hii leo ni Rob Holding, Ainsley Maitland-Niles na Jeff Reine.

No comments

Powered by Blogger.