Header Ads

Antonio Conte Awatoa Hofu Mashabiki Chelsea


Meneja wa vinara wa ligi ya nchini England (PL) Chelsea Antonio Conte amesisitiza kuwa, mshambuliaji kutoka nchini Hispania Diego Costa hatoondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu.

Mshambuliaji huyo mzaliwa wa nchini Brazil, alizua tafrani wakati wa dirisha dogo la usajili kwa kutaka kuhamia nchini China, ambapo alipata ofa nzuri.

Conte amezungumzia na shirika la utangazaji la Uingereza BBC, na kueleza suala la Costa limeshafikia pazuri, na ana uhakika mshambuliaji huyo hatokua na mshawasha wa kutikisa kibiriti kwa mara ya pili.

Amesema Diego Costa ni mchezaji muhimu kwenye kikosi chake, na ataendelea kumpigania kila kukicha, ili kufanikisha mpango wa kuendelea kuwa nae.

“Kila kitu kimekaa vizuri kwa sasa. Anafurahia maisha ya hapa. Anataka kuendelea kuwa nasi ili kusaka mafanikio makubwa zaidi.


“Nimepigana kwa kila hali kwa ajili ya kumshawishi ili abaki hapa, na ninafurahi kusema ameonyesha kukukubaliana na mimi, na ninaendelea kuahidi kwamba nitaendelea kumpigania.” Alisema Conte

No comments

Powered by Blogger.