Header Ads

Andre Marriner Kuamua Fainali Ya EFL Cup


Mwamuzi Andre Marriner ametajwa na chama cha soka nchini England FA, kwa ajili ya kusimamia sheria 17 za mchezo hatua ya fainali ya kombe la ligi (EFL CUP), kati ya Man Utd dhidi ya Southampton ambao utachezwa katika uwanja wa Wembley Jijini London Februari 26.

Marriner, mwenye umri wa miaka 46, atasaidiwa na Richard West na Stuart Burt wakati Kevin Friend atakua mwamuzi wa Akiba.
Msimu huu, katika Michezo 24 aliyochezesha, mwamuzi Marriner ametoa Kadi za Njano 92 na Nyekundu 5.


Mapema mwanzoni mwa Msimu huu, Marriner aliiminya Man Utd Penati ya wazi walipotoka Sare bao moja kwa moja dhidi ya Arsenal katika uwanja wa Old Trafford kwenye mchezo wa ligi kuu ya soka nchini England (PL).

No comments

Powered by Blogger.