Header Ads

Alaves Wavunja Mwiko Hispania, Waifuata FC Barcelona


Klabu ya Alaves imetinga kwenye hatua ya fainali ya kombe la Mfalme kwa mara ya kwanza, baada ya miaka 96 ya historia ya klabu hiyo.

Alaves imetimiza azma ya kufika kwenye hatua hiyo muhimu, kwa kuifunga Celta Vigo bao moja kwa sifuri katika mchezo wa mkondo wa pili wa hatua ya nusu fainali uliounguruma usiku wa kuamkia hii leo.

Kiungo mshambuliaji Edgar Mendez alifunga bao pekee na la ushindi la Alaves, baada ya kupokea pasi maridadi  kutoka kwa mlinda mlango Sergio Alvarez kwenye dakika ya 83.

Kabla ya kufungwa kwa bao hilo, mchezaji wa zamani wa Liverpool Lago Aspas, alikaribia kuiandikia Alaves bao la kuongoza, lakini umakini wa mlinda mlango Fernando Pacheco ulifuta mpango huo.

Alaves watacheza na FC Barcelona katika mchezo wa hatua ya fainali mwezi Mei mwaka huu.

Barcelona waliifunga Altetico Madrid mabao mawili kwa moja kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza, na katika mchezo wa mkondo wa pili uliounguruma Nou Camp usiku wa kuamkia jana walilazimisha sare ya bao moja kwa moja.


Kwa mara ya mwisho Alaves kucheza fainali ilikua mwaka 2001 katika michuano ya UEFA Cup, na waliambulia kisago cha mabao 5-4 dhidi ya Liverpool.

No comments

Powered by Blogger.