Header Ads

Ahmad Ahmad Azindua Ilani Ya Uchaguzi

Tokeo la picha la Ahmad Ahmad - Madagascar
Mpinzani wa rais wa shirikisho la soka barani Afrika CAF Issa Hayatou katika uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo utakaofanyika mwezi ujao mjini Adis Ababa nchini Ethiopia Ahmad Ahmad, amezindua ilani yake.
Ahmad aliepewa baraka za kuwania nafasi ya uras wa CAF na baraza la vyama vya soka kusini mwa Afrika (COSAFA) amezundua ilani hiyo, ambayo inayoonyesha mambo atakayoyafanya endapo atachaguliwa katika mkutano mkuu wa CAF.
Ahmad ambaye ni rais wa chama cha soka nchini Madagascar, anaaminiwa kuwa mpinzani wa kweli dhidi ya Hayatou ambaye amekua madarakani tangu mwaka 1988.
Katika ilani ya mgombea huyo, jambo kubwa ambalo ameliahidi ni kurekebisha utaratibu wa uongozi wa juu wa CAF na kufanya kazi zake kwa na uwazi.
Mambo mengine ambayo ameyapa kipaumbele ni:
Kulitangaza soka la Afrika kwa vitendo na kuyafanya mataifa ya bara hilo kuwa na uwezo wa kupambana na mataifa mengine ulimwenguni.
Kukuza soka la Afrika na kujenga ujasiri kwa mataifa ya bara hilo.
Kuleta maridhiano ndani ya soka la Afrika.
Kuweka usawa kati ya mataifa ya Afrika.

Kujenga miundombinu ambayo itakua chachu ya kuendeleza soka la Afrika.

No comments

Powered by Blogger.