Header Ads

AFCON 2017: CAF Yataja 11 Bora


Wachezaji wa timu ya taifa ya Ghana Christian Atsu na Daniel Amartey wametajwa katika kikosi cha AFCON 2017 (CAF Best XI for the 2017 Africa Cup of Nations).

Atsu, ambaye anaitumikia klabu ya Newcastle Utd ya nchini England, ametajwa kuwa sehemu ya viungo watano walioteuliwa katika kikosi hicho, baada ya kuonyesha uwezo mkubwa wa kusakata soka wakati wa fainali za AFCON 2017, zilizomalizika mwishoni mwa juma lililopita.

Hii inakua ni mara ya pili mfululizo kwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25 kutajwa katika kikosi bora cha wachezjai 11 wa Afrika mara baada ya fainali za AFCON, mwaka 2015 alitwajwa baada ya fainali hizo kumalizika huko Equatorial Guinea.

Kwa upande wa mabingwa wa soka barani Afrika mwaka 2017, timu ya taifa ya Cameroon wametoa wachezaji watatu kwenye kikosi hicho ambao ni Fabrice Ondoa, Michael Ngadeu na Christian Bassogog.

Kikosi kamili cha wachezaji walioteuliwa na kamati ya ufundi ya shirikisho la soka barani Afrika CAF.

Kipa: Fabrice Ondoa (Cameroon)

Mabeki: Modou Kara Mbodji (Senegal), Ahmed Hegazy (Egypt) Na Michael Ngadeu (Cameroon)

Viungo: Charles Kabore (Burkina Faso), Daniel Amartey (Ghana), Bertrand Traore (Burkina Faso), Christian Atsu (Ghana) Na Mohamed Salah (Egypt)

Washambuliaji: Christian Bassogog (Cameroon) Na Junior Kabananga (Dr Congo)

No comments

Powered by Blogger.