Header Ads

Adele akili beyonce ni zaidi yake, ammpa tuzo yake

Tokeo la picha la Adele

Nyota wa muziki nchini Marekani  Adele ameonekana kukataa tuzo ya Grammy aliyotunukiwa kwa kuwa na albamu bora zaidi.

Badala yake, amesema Beyonce ndiye aliyestahili zaidi kutunukiwa tuzo hiyo.
Adele alipewa tuzo hiyo kwa albamu yake kwa jina 25 ambayo imevuma sana duniani, lakini amewaambia waliohudhuria kwamba, "Haiwezekani kwangu kupokea tuzo hii".

"Ni heshima kubwa sana kwangu na nashukuru, lakini Beyonce ndiye mwanamuziki bora maishani mwangu".

Miaka miwili iliyopita,katika tuzo za grammy Kanye West aliondoka kwa hasira jukwaani baada ya Beyonce kukosa kutangazwa mshindi kwa albamu yake ijulikanayo kwa jina la Beck's Morning Phase.

Ushindi wa Adele dhidi ya Beyonce bila shaka utachocheza zaidi malalamiko kwamba tuzo za Grammy sana huwabagua wasanii weusi.

Baadhi ya wasanii wakiwemo Frank Ocean na Kanye West, waliamua kususia sherehe za mwaka huu za kutoa tuzo kwa washindi kwa msingi huo.

Beyonce katika tuzo za Grammys

No comments

Powered by Blogger.