Header Ads

Umoja Wa Mataifa Watoa Wito Wa Mbinu Mpya Ya Kutimiza Maendeleo Na Amani


Umoja wa Mataifa umetoa wito wa mbinu mpya itakayoboresha maendeleo na kuzuia migogoro kwa kukabiliana na vyanzo vyake na kudumisha amani.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw Antonio Guterres amesema hayo kwenye mjadala wa ngazi ya juu kuhusu kujenga amani ya kudumu duniani.
Amesema utekelezaji wa ajenda ya maendeleo endelevu ambayo inajumuisha malengo kadhaa ya kuondoa umaskini, kuboresha usawa wa jinsia na kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa kutatoa mchango mkubwa katika kudumisha amani.

Ajenda ya Maendeleo ya Mwaka 2030 ilipitishwa mwezi Septemba mwaka 2015 na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, ili kuongoza maendeleo na ushirikiano wa kimataifa hadi mwaka 2030.

No comments

Powered by Blogger.