Header Ads

Umoja Wa Mataifa Kujenga Uhusiano Mpya Na Umoja Wa Afrika


Msemaji wa Umoja wa mataifa Stephane Dujarric amesema katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterress atakwenda Addis Ababa, nchini Ethiopia kuhudhuria mkutano wa kilele wa 28 wa Umoja wa Afrika.

Dujarric amesema kwenye mkutano huo Bw Antonio Guterress atatoa wito wa kujenga uhusiano mpya wa ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika, kwenye msingi wa kuheshimiana na kushikamana, na kufuatilia kwa pamoja masuala yanayohusiana na malengo ya maendeleo endelevu na utekelezaji wa Ajenda 2063 kwa Afrika.


Dujarric ameongeza kuwa Guterress anatarajiwa kukutana na viongozi wa nchi za Afrika watakaohudhuria mkutano huo, na pia atakutana na mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Ethiopia.

No comments

Powered by Blogger.