Header Ads

Umoja Wa Afrika Watoa Tuzo Kwa Wanasayansi


Wanasayansi watano wa kike wa Afrika wamepewa tuzo za kikanda za Kwame Nkrumah za mwaka huu zilizoandaliwa na Umoja wa Afrika.
Sherehe ya kukabidhi tuzo ilifanyika katika mkutano wa jinsia ukiwa sehemu ya mkutano wa 28 wa kilele wa Umoja wa Afrika unaofanyika huko Addis Ababa.
Tuzo za kisayansi za Kwame Nkrumah za Umoja wa Afrika zinakabidhiwa kwa wanasayansi hodari wa Afrika katika ngazi za kitaifa, kikanda na kibara.

Tuzo hizo za kikanda zinalenga kuhimiza ushiriki wa wanawake wa Afrika katika sayansi na teknolojia.

No comments

Powered by Blogger.