Header Ads

Uchaguzi Wa Rais Somalia Kufanyika Februari 8


Uchaguzi wa rais wa Somalia utafanyika tarehe 8 mwezi ujao katika kikao cha pamoja cha bunge, chini ya usimamizi wa tume mpya ya uchaguzi.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Abdirahman Dualeh Beileh amesema uandikishaji wa wagombea urais unaanza leo hadi Jumapili wiki hii.

Somalia inatarajiwa kufanya uchaguzi huo kwa njia isiyo ya moja kwa moja ambayo wabunge watachagua kiongozi mpya wa nchi, baada ya uchaguzi wa rais kuahirishwa mara kadhaa kwa mwaka jana.

Timu ya uchaguzi itafanya mikutano miwili kujadili muundo wa uchaguzi. Orodha ya maseneta na wabunge 17 watakaoshiriki kwenye tume mpya ya uchaguzi imetangazwa.


Jumuiya ya kimataifa imetaka uchaguzi huo uwe wa haki, huru na wa kuaminika.

No comments

Powered by Blogger.