Header Ads

Tunajiandaa Kwa ‘Dabi’ Ya Mbeya


Baada ya  ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kabela City FC ya Shinyanga kwenye kombe la shirikisho hapo jana, kikosi cha Mbeya City FC hii leo kimeanza mazoezi kujindaa na mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara dhidi ya Tanzania Prison  uliopangwa  kuchezwa mwishoni mwa juma hili kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Kocha  msaidizi wa kikosi hiki Mohamed Kijuso ameimbia mbeyacityfc.com kuwa  maandalizi kuelekea mchezo  huo wa jumamosi yanaenda vizuri na wachezaji wote wako kwenye hali nzuri, kinachofanyia  sasa ni kurekebisha makosa  yaliyojitokeza kwenye mchezo wa kombe la FA licha ya kupatikana kwa ushindi wa bao 2-0.

Tunashukuru Mungu  kwa sababu tulipata matokeo kwenye mchezo wa kombe la FA hapo jana licha ya mchezo kuwa mgumu, tuko mazoezini hivi sasa kurekebisha makosa yote yalitokea  hii ni sehemu ya maandalizi yetu kuelekea  mchezo ujao,kwa mujibu wa daktari vijan wangu wote wako fiti, naiheshimu Tanzania Prison ni timu nzuri  huwezi kuibeza kwa namna yoyote,  ni wazi mchezo wa jumamosi utakuwa mgumu.

Akiendelea  zaidi Kijuso alisema kuwa mipango na malengo ya kikosi chache ni kuhakikisha   wanakuwa sehemu ya timu nne za juu kwenye msimamo wa ligi  mara ifikapo mwisho wa msimu.

Mara kadhaa nimekuwa nikisema nia  yetu ni kuwa  sehemu ya timu nne za juu mwisho wa msimu,hili litawezekana kwa sababu nafasi bado tunayo, nina imani kubwa na vijana wangu kwa sababu sasa wako kwenye kiwango kizuri, kitu pekee naomba mashabiki wetu  watusapoti kwa nguvu zote kama ambavyo wamekuwa wakifanya kwenye michezo iliyopita.

Kuhusu suala la waamuzi kutupiwa lawama kwa kushindwa kutafsiri kwa ufasaha sheria 17 za soka, Kijuso alikataa kuzungumza lolote kwa madai kuwa waamuzi ni binadamu hivyo  kuna wakati lazima watafanya makosa  kama  ilivyo kwa watu wengine na kutoa wito wa kujirekebisha pale wanapotuhumiwa.

No comments

Powered by Blogger.