Header Ads

Siku Ya Kwanza Ya Mkutano Wa Astana Yamalizika Kwa Mivutano


Siku ya kwanza ya mkutano wa siku mbili wa Astana kuhusu mgogoro wa Syria ilimalizika kwa wajumbe wa serikali na wa upinzani kufanya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja, huku mivutano ikidhihirika.
Ujumbe wa serikali na waasi ulikutana ana kwa ana kwa muda mfupi, ikiwa ni mara ya kwanza kwa muda wa miaka sita tangu mgogoro uanze.
Uturuki, Iran na Russia pia zilihudhuria mkutano huo, hata hivyo mkutano huo ulichelewa kwa muda wa dakika 40 kutokana na baadhi ya waasi kutoafiki uwepo wa ujumbe wa Iran kwenye mkutano.
Moja ya mambo yaliyokuwa magumu kwenye mkutano huo, ni mada kuhusu kundi la Al Nusra Front lenye uhusiano na kundi la Al Qaeda ambalo limebadilisha jina.

Waasi wanaona si haki kuliona kundi hilo kama ni adui.

No comments

Powered by Blogger.