Header Ads

Ronald Koeman Kuungana Na Schneiderlin Goodison Park


Kiungo Morgan Schneiderlin yu njiani kuondoka Old Trafford kwa ada ya uhamisho ya Pauni milion 22.
Klabu ya Everton inapewa nafasi kubwa ya kukamilisha usajili wa kiungo huyo ambaye amekua hapati nafasi ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza.
Gazeti la The Sun la nchini England limeripoti kuwa, tayari Man Utd wameshakubali ofa iliyowasilishwa mezani kwao, na wakati wowote huenda taratibu za uhamisho wa Schneiderlin zikafuata mkondo.
Gazeti hilo limeeleza kuwa, Man Utd walihitaji kiasi cha pauni milioni 24 ili kumuachia Schneiderlin, lakini Everton waliwashusha na kufikia Pauni milioni 22, na ndani ya saa 48 zijazo huenda The Toffees wakammiliki kiungo huyo.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27, anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya katika kituo cha mazoezi cha Everton kiitwacho “Finch Farm Training Ground”.
Ronald Koeman 

Uzito wa usajili wa Schneiderlin, umepatikana kufuatia uwepo wa meneja Ronald Koeman huko Goodison Park, na mahusiano ya urafiki kwa wawili hao tangu walipokua St Marries yanatajwa kunogesha taratibu hizo.

No comments

Powered by Blogger.