Header Ads

Real Madrid Waendelea Kutanua Kileleni


Vinara wa ligi kuu ya soka nchini Hispania (La Liga), klabu ya Real Madrid wameibanjua Real Sociedad katika mchezo wa ligi ya nchini humo, uliochezwa usiku wa kuamkia hii leo kwenye uwanja wa Bernabeu mjini Madrid.

Mabao ya Real Madrid yalifungwa na Mateo Kovacic, Cristiano Ronaldo pamoja na Alvaro Morata katika dakika ya 38, 51 na 82.

Ushindi huo umeiwezesha Real Madrid kuendelea kuongoza ligi kwa tofati la point 4 dhidi ya mahasimu wao FC Barcelona ambao mapema jana walilazimishwa sare ya bao moja kwa moja dhidi ya Real Betis.

Real Madrid wamefikisha point 46 na FC Barcelona wanamiliki point 42 sambamba na Sevilla CF wanaoashika nafasi ya tatu.

Atletico Madrid wapo kwenye nafasi ya nne kwa kufikisha point 36.
Michezo mingine ya ligi kuu ya soka nchini Hispania iliyochezwa jana.

Espanyol 3 – 1 Sevilla

Athletic Bilbao 2 – 1 Sporting Gijon

No comments

Powered by Blogger.