Header Ads

Pauni Laki 3 Zapatikana Kuwachangia Chapecoense

Kiasi cha pauni laki 3 kimechangishwa kwenye mchezo wa kirafiki, pale Brazil ilipoifunga Colombia 1-0 katika mchezo wa kusaidia familia za wachezaji na wafanyakazi wa klabu ya Chapecoense waliofariki kwenye ajali ya ndege.
Katika mchezo huo uliopigwa alfajiri ya jana kwa masaa ya Afrika Mashariki, mshambuliaji, Dudu aliwafungia Brazil bao kabla ya mapumziko, katika uwanja wa Olimpiki mjini Rio.
Chapecoense walitoka 2-2 na Palmeiras, kwenye mchezo wa kirafiki Jumamosi iliyopita ikiwa na kikosi kipya kilichosajiliwa baada ya miezi miwili ya kupoteza wachezaji wake kwenye ajali iliyotokea mwezi Novemba mwaka jana.

Watu 6 pekee ndiyo waliobaki katika msafara wa watu 77 waliokuwemo kwenye ndege ya LaMia iliyobeba wachezaji wa Chapecoense ikielekea Colombia kucheza fainali ya Copa Sundamericana.

No comments

Powered by Blogger.