Header Ads

Olympic Marseille Yamrejesha Nyumbani Patrice Evra


Beki wa kushoto kutoka nchini Ufaransa na klabu ya Juventus ya Italia Patrice Evra amejiunga na klabu ya Olympic Marseille kwa mkataba wa miezi 18.

Klabu ya Olympic Marseille yenye maskani yake mjini Marseille nchini Ufaransa imethibitisha kukamilika kwa taratibi zote za uhamisho wa mchezaji huyo, ambaye aliwahi kutamba na Man Utd ya England.

Kabla ya mpango wa kusajiliwa na Olympic Marseille haujakamilishwa, beki huyo mwenye umri wa miaka 35 alikua nahusishwa na taarifa za kutaka kurejea nchini England ili kujiunga na na Man Utd ama Crystal Palace na taarifa nyingine zilieleza alikua anawaniwa na klabu ya Valencia ya Hispania.


Mkataba wa Evra na Juventus ulikua unafikia kikomo mwishoni mwa msimu huu, hivyo suala la kuondoka kwake limeinufaisha klabu hiyo ya mjini Turine.

No comments

Powered by Blogger.