Header Ads

Ni Zamu Ya Adam David Lallana


Uongozi wa klabu ya Liverpool upo kwenye harakati za kumsainisha mkataba mpya kiungo mshambuliaji Adam David Lallana.

Liverpool wamejipanga kukamilisha mpango huo kwa kumsainisha Lallana mkataba wa miaka miwili.

Mkataba wa sasa wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28, unafikia kikomo mwaka 2019, na kama atakubaliana na viongozi wa Liverpool atakua na nafasi ya kuendelea kusalia Anfield hadi mwaka 2021.

Kama mambo yatakwenda vyema, Lallana atakua akipokea mshahara wa Pauni 150,000 kwa juma, ambao ni mara mbili ya mshahara anaolipwa sasa.


Juma lililopita uongozi wa Liverpool ulifanikisha mpango wa kumuongezea mkataba kiungo mshambuliaji kutoka nchini Brazil Philippe Coutinho Correia, ambaye ataendelea kuwepo Anfield hadi mwaka 2022.

No comments

Powered by Blogger.