Header Ads

Ni Serena Williams Na Venus Williams

Ndugu wawili raia wa Marekani Serena na Venus Williams watakutana kwenye fainali ya Grand Slam kwa mara ya tisa kunako michuano ya wazi ya Australia kufuatia wanadada hao kushinda mechi zao za nusu fainali.
Venus aliye katika nafasi ya tatu kwenye viwango vya ubora duniani ametinga fainali ya grand slam kwa mara ya kwanza tangu 2009 kwa kumnyuka Coco Vandeweghe kwa aseti 6-7, 6-2 na 6-3 huku Serena anayewania taji la grand slam kwa mara ya 23 amemshinda mcroatia Lucic-Baroni kwa seti 6-2 6-1 katika mchezo uliochezwa jana.
Hii ni mara ya kwanza kwa ndugu hao kukutana katika fainali ya mashindano ya grand slam katika kipindi cha miaka 8 ambapo kwa mara ya mwisho ilikuwa ni mwaka 2009 katika mashindano ya Wimbledon na Serena alipata ushindi.

Mchezo huu utapigwa siku ya Jumamosi, Februari 28 na baadhi ya wadau na wataalamu wa mchezo huo wametabiri ugumu wa mchezo wa fainali hiyo. 

No comments

Powered by Blogger.