Header Ads

Michael Olunga Kujiunga Na Klabu Ya China


Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars Michael Olunga amejiunga na klabu iliopandishwa daraja katika ligi ya China Guizhou HengFeng Zhicheng kutoka kwa klabu ya Djurgadens IF ya Sweden.


Olunga mwenye umri wa miaka 22 aliachiliwa na Djurgadens IF baada ya vilabu vyote viwili kukubaliana.

Kulingana na gazeti la The Standard nchini Kenya, Olunga alikuwa amesalia na miaka mitatu katika mkataba yake.

Mchezaji huyo aliifungia Gor Mahia mabao 19 katika msimu wa 2015, na kuwasaidia kushinda taji la 15 la KPL pamoja na taji la Top 8 kabla ya kujiunga na klabu hiyo ya Sweden.

Mchezaji huyo wa zamani wa Gor Mahia na Tusker pia amekuwa akisakwa na klabu ya Urusi ya CSKA Moscow pamoja na Galatasaray ya Uturuki.

No comments

Powered by Blogger.