Header Ads

Memphis Depay Yu Njiani kuondoka Old TraffordMshambuliaji kutoka nchini Uholanzi Memphis Depay, ana matumaini makubwa ya kuondoka Old Trafford katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili.

Depay ameibua matumaini hayo, kufuatia hali ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Mana Utd kuwa ngumu kwake, tangu alipowasili Jose Mourinho mwanzoni mwa msimu huu.

Klabu ya Olympique Lyon ya nchini Ufaransa inatajwa kuwa katika mpango mzuri wa kumsajili mshambuliaji huyo, ambaye alitua Old Trafford wakati wa utawala wa Louis Van Gaal.

Lyon na Man utd zimeripotiwa kuwa katika mazungumzo ya usajili wa Depay mwenye umri wa miaka 22, na kama mambo yatakwenda vyema mambo yatawekwa hadharani.


Man Utd walimsajili Depay akitokea PSV Eindhoven, na katika msimu miwili ya mwanzo alipata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza.

No comments

Powered by Blogger.