Header Ads

Marc-Andre ter Stegen Awekwa Njia Panda


Mustakabali wa mlinda mlango wa FC Barcelona Marc-Andre ter Stegen upo shakani kufuatia mazungumzo ya kusaini mtakaba mpya kusitishwa.

Jarida la michezo nchini Hispania la Don Balon limeripoti kuwa, mazungumzo ya kusainiwa kwa mkataba mpya wa mlinda mlango huyo yamesitishwa kutokana na kazi nzito inayoukabili uongozi wa FC Barcelona kwa sasa.

FC Barcelona wanahaha kuwabakisha Andrés Iniesta, Ivan Rakitic pamoja na Lionel Messi, hivyo wameona ni bora kushughulika na wachezaji hao kwanza na kumuweka pembeni kwa muda Ter Stegen.

Mkataba wa mlinda mlango huyo kutoka nchini Ujerumani, unatarajia kufikia kikomo 2019.

Hata hivyo jarida hilo limeongeza kuwa, katika vikao vya ndani ya klabu hiyo mazungumzo ya kusakwa kwa mlinda mlango mpya yanaendelea, hali ambayo bado inahatarisha uwepo wa Ter Stegen.


Tetesi za awali zimedai kuwa mlinda mlango chaguo la kwanza la klabu ya Benfica ya nchini Ureno Ederson Santana de Moraes raia wa Brazil, anapigiwa chepuo la kusajili itakapofika mwishoni mwa msimu huu.

No comments

Powered by Blogger.