Header Ads

Manolo Gabbiadini Kutua Southampton


Klabu ya Southampton imekubali kulipa Pauni milioni 17, kwa ajili ya usajili wa mshambuliaji wa klabu ya Società Sportiva Calcio Napoli Manolo Gabbiadini.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25, aliwekwa sokoni kufuatia hali kumuendelea kombo, kufuatia uwepo wa washambuliaji wengine kama Arkadiusz Milik na Dries Mertens ambao wanapata nafasi ya kucheza mara kwa mara.

Mpango wa usajili wa Gabbiadini unatarajiwa kukamilishwa hii leo, na makubaliano ya awali yanaitaka klabu ya Southampton kutoa Pauni milioni 14.6 na kisha watamalizia kiasi cha Pauni milioni 2.6 endapo kiwango cha mshambuliaji huyo kitawaridhisha.


Gabbiadini alitarajiwa kusafiri hadi nchini England usiku wa kuamkia hii leo, kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya.

No comments

Powered by Blogger.