Header Ads

Makamu Wa Rais Awapongeza Black Stars

Makamu wa rais wa Ghana Mahamudu Bawumia ametuma salamu za pongezi kwa wachezaji wa timu ya taifa ya nchi hiyo, kufuatia hatua ya kufuzu kucheza nusu fainali ya AFCON 2017 dhidi ya Cameroon.
Bawumia amesema wachezaji wa Black Stars walistahili kupata ushindi mbele ya Congo DRC, kutokana na soka safi walilolionyesha, huku akisisitiza kutaka kuona mazuri yakiendelezwa kwenye timu hiyo.
Amesema hakuna litakalowashinda wachezaji wa timu ya taifa lake, kwa kisingizio cha kuzidiwa mbinu, kwani anaamini benchi la ufundi lina kila sababu ya kupanga mikakati ya kumaliza mambo yote uwanjani.
Akizungumza mchezo dhidi ya Cameroon ambao utacheza siku ya Al-khamisi, Bawumia amesema hana shaka kutokana na kukiamini kikosi cha Ghana kilichosheheni wachezaji wengi wenye uzoefu mkubwa.

Ghana watacheza dhidi ya Cameroon katika mchezo wa pili wa nusu fainali siku ya Al-khamis.

No comments

Powered by Blogger.