Header Ads

Mahakama Kuu Ya Ugiriki Yaamua Kutowarejesha Askari 8 Wa Uturuki


Mahakama kuu ya Ugiriki imefanya uamuzi wa kutowarejesha askari 8 wa Uturuki wanaotuhumiwa kushiriki kwenye jaribio la mapinduzi ya kijeshi lililotokea mwezi Julai mwaka jana.

Baada ya jaribio la mapinduzi ya kijeshi tarehe 15 mwezi Julai, askari 8 wa Uturuki walikimbilia Ugiriki kwa helikopta na kukamatwa na polisi wa Ugiriki.


Mwezi Agosti Uturuki iliitaka Ugiriki iwarejeshe askari hao ambao walishitakiwa kushiriki kwenye jaribio la mapinduzi ya kijeshi. Lakini askari hao wanane walikana mashitaka hayo.

No comments

Powered by Blogger.