Header Ads

Lukuvi Aanza Kugawa Neema Kwa Wananchi


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, ameendelea na ziara yake ya utatuzi wa migogoro ya ardhi ambapo amewapatia wananchi wa kijiji cha kinywang'anga Iringa vjijini,hati za umiliki ardhi zaidi ya 800.

Katika ziara hiyo, Lukuvi amekutana na wanakijiji hao waliopimiwa maeneo yao ya viwanja na mashamba ambao kwa sasa hati zao za umiliki wa ardhi zimeshaandaliwa.

Aidha ziara hiyo ni utekelezaji wa programu ya kitaifa ya kupima na kumilikisha ardhi na kuzuia migogoro ya ardhi wenye lengo la kufanyika nchi nzima.

Hata hivyo utekelezaji huo utahusisha kuhakiki mipaka ya mitaa na vijiji na maeneo mengine yote na kupima kila kipande cha ardhi.

Sambamba na hilo matangazo ya Serikali yanayotambulisha mipaka ya mikoa, wilaya, hifadhi za Taifa na vijiji yatafanyiwa marekebisho baada ya mipaka yote kuhakikiwa.

No comments

Powered by Blogger.