Header Ads

Kenya Imepokea Kundi La Pili La Treni Za Abiria


Kundi la pili la vichwa vya treni za abiria na mizigo ya kiwango cha SGR vimewasili katika bandari ya Mombasa.

Hadi sasa Kenya imepokea jumla ya vichwa 10 vya treni baada ya kundi la kwanza la vichwa vya treni 6 kuwasili majuma mawili yaliyopita ikiwa ni sehemu ya vichwa 56 ambavyo vinatarajiwa kuwasili nchini humo kabla ya Juni 1 mwaka huu.

Mkurugenzi wa shirika la reli Atanas Maina amesema kuwasili kwa vichwa hivyo kutasaidia kupata muda wa kujaribu injini pamoja na reli na baada ya majaribio hayo, zitaanza kufanya kazi kwa kusafirisha abiria pamoja na mizigo.

Kampuni ya ujenzi wa barabara na madaraja ya China (CRBC) imetekeleza mradi huo wa SGR ambao ulianzishwa na kuwezesha jumla ya wakenya 30,000 kupata ajira na kusaidia moja ya changamoto kubwa ya ajira nchini humo.


Rais Uhuru Kenyatta anatarajia kuzindua rasmi mradi huo Mei 31 mwaka huu.

No comments

Powered by Blogger.