Header Ads

Federer Atinga Nusu Fainali Ya Australia Open


Mkongwe Roger Federer amefuzu kwa nusu fainali ya mashindano ya wazi ya tennis ya Australia baada ya kumlaza Mischa Zverev kwa seti tatu kwa bila ndani ya dakika 92 tu.

Federer ametinga kwenye nusu fainali yake ya 13 ya michuano hiyo baada ya kushinda kwa 6-1, 7-5 na 6-2 na sasa atacheza na nduguye wa Taifa moja Stan Warwinka aliyemtoa Jo-Wilfred Tsonga.

Wengi walitaraji Mischa Zverev angempa upinzani mkubwa Federer hasa baada ya kumtoa Andy Murray siku ya Jumapili, na Stan Warwinka alimfunga Mfaransa Tsonga kwa seti tatu kwa bila kwa ushindi wa 7-6, 6-4 na 6-2.


Kwa upande wa akina dada nguli mwingine Venus Williams nae amefuzu kwa nusu fainali ya mashindano hayo baada ya miaka 14 kupita baada ya kumtoa Anastasia Pavlyuchenkova wa Russia katika hatua ya robo fainali, na sasa atacheza na Coco Vandeweghe ambaye alimshinda Garbine Muguruza kwenye robo fainali kwa seti mbili kwa bila.

No comments

Powered by Blogger.