Header Ads

FA Cup: Ratiba Ya Mzunguuko Wa Tano Hadharani


Klabu ya Sutton inayoshiriki madaraja ya chini katika soka la nchini England, imepangwa kuwa mwenyeji wa washika bunduki wa Ashburton Grove (Arsenal) katika mzunguuko wa tano wa michuano ya kombe la FA.

Sutton wametinga katika mzunguuko wa tano na kupangwa kukutana na Arsenal, baada ya kuifunga Leeds Utd katika mchezo wa mzunguuko wa nne uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita.

Klabu nyingine ambayo inashiriki madaraja ya chini iliyotinga katika mzunguuko wa tano wa michuano ya kombe la FA ni Lincoln City ambayo imepangwa kukutana na Burnley.

Hii ni mara ya kwanza katika historia ya michuano ya kombe la FA kuwa na timu za madaraja ya chini inapofikia hatua ya mzunguuko wa tano.

Ratiba ya michezo mingine iliyopangwa usiku wa kuamkia hii leo na chama cha soka nchini England (FA), inaonyesha wababe wa majogoo wa jiji Liverpool, Wolverhampton Wanderers wamepangwa kukutana na Chelsea. 

Oxford ambao waliwatupa nje ya michuano hiyo Newcastle Utd, watasafiri hadi Riverside Stadium kupambana na Middlesbrough.

Baada ya kunusurika mbele ya Wycombe Wanderers katika mchezo wa mzunguuko wa nne, Tottenham Hotspurs wamepangwa kukutana na wenzao wa jijini London Fulham, huku mabingwa watetezi Manchester United na majirani zao Manchester City watasafiri katika miji ya karibu kupambana an Blackburn na Huddersfield.

Ratiba kamili ya mzunguuko wa tano iliyopangwa usiku wa kuamkia hii leo.

Burnley v Lincoln City
Fulham v Tottenham Hotspur
Blackburn Rovers v Manchester United
Sutton United v Arsenal
Middlesbrough v Oxford United
Huddersfield Town v Manchester City
Wolverhampton Wanderers v Chelsea
Millwall v Derby County au Leicester City

Michezo ya mzunguuko wa tano ya kombe la FA imepangwa kuchezwa Februari 18.

No comments

Powered by Blogger.