Header Ads

Chelsea Yamnyatia Jackson MartinezKlabu ya Chelsea imetuma ofa ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Atletico Madrid Jackson Martinez ambaye kwa sasa anaitumikia Guangzhou Evergrande.

Wakala wa mshambuliaji huyo kutoka nchini Colombia ameanza kushughulikia suala hilo, ili kuangalia uwezekano wa kuona mchezaji wake anawahi muda wa usajili wa dirisha dogo.

Chelsea wametumia nafasi ya kutuma ofa ya kumsajili Martinez, kwa kigezo cha mchezaji huyo kushindwa kutumika ipasavyo chini ya kocha  Luiz Felipe Scolari.

Scolari hajamjumuisha Martinez katika orodha ya wachezaji watakaoshiriki ligi ya mabingwa barani Asia kwa msimu huu, hali ambayo imemkatisha tamaa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30.


Mtandao wa Tribalfootball.com umeripoti kuwa, mbali na Chelsea klabu nyingine za nchini England kama West Ham na Leicester City zipo kwenye purukushani za kuiwania saini ya Martinez.

No comments

Powered by Blogger.