Header Ads

Afrika Kusini Yakanusha Habari Kuhusu Vichwa Vya Treni Vya China


Kampuni ya reli ya Afrika Kusini Transnet imekanusha habari za uwongo na kusema inaridhika na ubora wa vichwa vya treni vilivyoagizwa kutoka China.
Baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kuwa vichwa hivyo vilikuwa na hitilafu za kiufundi, na kampuni ya Transnet ilikataa kupokea vichwa vingine 18 kutoka China kutokana na sababu hiyo.

Meneja mawasiliano wa kampuni hiyo Bw Molatwane Likhethe amesema, ripoti hizo hazina msingi wowote.

No comments

Powered by Blogger.